Wakaazi wa Transmara waombwa kuwaheshimu wahudumu wa afya 

Gavana wa kaunti ya Narok, Patrick Ole Ntutu amewaonya wakaazi wa gatuzi dogo la Transmara Magharibi dhidi ya kushambulia, kuzuia au kutekeleza aina yoyote ya ghasia kwa mtumishi wa umma anayetoa huduma kwa umma kihalali. Ntutu alisema kuwa yeyote yule atakayepatikana katika makosa ya aina hii basi bila shaka atachukuliwa hatua ya kisheria kwa kukamatwa…